mastar mbalimbali wa Tanzania wamekua wakionyesha magari yao ambayo mengi yamekua ya kifahari,kwa mwaka 2014 ni mwaka unaonyesha wasanii wengi kumiliki magari ya gharama zaidi,mpaka sasa ni zaidi ya wasanii watano ambao wameonyesha magari yao ya kifahari.
Star wa single mbalimbali ikiwemo Nakula Ujana Ney wa Mitego nae yupo kwenye list ya wasanii wanaomiliki magari haya ya thamani hii ya Ney wa Mitego ni Nissan Morano ya mwaka 2007 na hii inakamilisha gari la pili kwenye kipindi kifupi baada ya ile Toyota Mark X.
Kwa maelezo ya mwenyewe Ney ingawa hakutaka kutaja bei kamili aliyonunulia lakini kasema ni zaidi ya Milioni 35 za Kitanzania,na hii aliinunua kama zawadi kwake siku ya June 09 alipokua anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Tag :
Gossip stories
0 Komentar untuk "Angalia mkoko mpya wa Ney Wamitego..... Ni noma sana"