Kusaidia watu ambao kweli wanahitaji msaada ni suala la msingi sana kwani wanafarijika na kujiona nao wana watu wanaowajali.
Mwanamuziki maarufu nchini, Naseeb Abdul, ‘Diamond’, amesema anapenda kusaidia jamii kuliko kustarehe.
Diamond alisema katika mahojiano na gazeti hili
kuwa anaposaidia jamii hukumbuka namna alivyowahi kusaidiwa, kwani
katika maisha yake kabla ya kufikia mafanikio aliyonayo sasa, alisaidiwa
sana na watu.
“Maumivu ya shida na uhitaji nayafahamu, ndiyo
maana nikiitwa kwenye shughuli yoyote ya kijamii nafarijika sana,
najikumbusha nilivyokuwa nahitaji msaada,” alisema Diamond.
Alisema hivi karibuni alikuwa Afrika Kusini
kwenye mradi maalumu wa kupinga njaa Afrika, ambako pamoja na mambo
mengine alikutana na wasanii wakubwa, alibadilishana nao mawazo na
kupata kitu kipya kutoka kwao.
“Wakati mwingine ukifanya jambo moja linazaa
lingine, ndiyo maana nasema ninaposaidia jamii kwa namna yoyote ile
hufarijika kuliko ninapofanya starehe,” alisema Diamond.
Diamond alisema akiwa katika mradi huo nchini
Afrika Kusini, alipata bahati ya kuzungumza na mkali wa muziki Afrika,
Yvonne Chakachaka na kujifunza mengi kutoka kwake.
“Siku hazigandi, ipo siku nitakaa kwa muda na
kuangalia tunaweza kufanya nini katika muziki na mwanamama huyu mwenye
mengi ya kujifunza, nilikaa naye kwa muda mfupi, lakini nilichojifunza
ni kama nimekaa naye mwaka mzima,”alisema Diamond.
Tag :
News
0 Komentar untuk "Diamond Platnum : Napenda kusaidia jamii kuliko starehe"