Zurich, Uswisi. Wakati wote kushinda tuzo ya
Ballon d’Or inatokana na ushindani wa hali ya juu nje ya uwanja kuwa
nani mwenye mvuto na kipaji binafsi.
Kwa miezi kadhaa iliyopita vita ilikuwa nani
anastahili kuwa mwanasoka bora kati ya nyota wawili, Cristiano Ronaldo
na Lionel Messi.
Kila moja alikuwa na mtazamo wake juu ya nani
anayestahili kushinda, japokuwa mwisho wa siku Cristiano Ronaldo
amefanikiwa kunyakua tuzo hiyo kwa kupata kura nyingi zaidi ya wenzake.
Kwa mujibu wa matokeo, Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Mfumo wa kupiga kura unafanywa kwenye tovuti ya
Fifa, kwa chaguo la kwanza ni pointi tano, pointi tatu kwa chaguo la
pili na pointi moja kwa chaguo la tatu, kwa kile kichotegemewa na wengi
si Messi wala Ronaldo aliyempigia kura mwenzake kuwa chaguo la kwanza.
Jambo la kushangaza ni wawili hao kutomchagua yeyote aliyekuwa kwenye orodha ya wachezaji watatu wa mwisho.
Kura hizo zilipigwa na manahodha wa timu za taifa, makocha na wanahabari wa nchi wanachama wa FIFA.
Nahodha wa Argentina na Ureno, Messi na Ronaldo waliruhusiwa kupiga kura, lakini hawakutakiwa kujipigia kura wenyewe.
Messi yeye alitoa kura zake kwa wachezaji wenzake wa Barcelona, alimpa kura ya kwanza Andres Iniesta, Xavi na Neymar.
Ronaldo yeye alimpa kura ya kwanza mshambuliaji wa
Colombia na Moncao, Radamel Falcao, huku nafasi ya pili akimpa Gareth
Bale pamoja na Mesut Ozil.
Messi atakuwa na jambo la kujadili na kocha wake
wa timu ya taifa Alejandro Sabella, aliyempa Ronaldo pointi muhimu kwa
kumchagua wa tatu, huku Messi akiwa wa kwanza na Franck Ribery.
Winga wa Bayern Munich alimaliza nafasi ya tatu,
huku nahodha wa Ufaransa, Hugo Lloris na kocha wake Didier Deschamps
wakimchagua Ribery kuwa wa kwanza.
Tag :
soccer
0 Komentar untuk "Christiano Ronaldo na Messi wanyimana kura barani ulaya"