Thursday, February 27, 2014

Bingwa mara mbili wa dhahabu katika Olimpiki, na ambaye pia ni bingwa wa
ulimwengu katika mbio za mita 10,000 na 5,000 Muingereza Mo Farah yuko
nchini Kenya lakini siyo kwa mapumziko au kujivinjari tu…hapana.
Mo Farah atakuwa nchini humo kwa kipindi cha wiki nne, ili kufanya
mazoezi makali katika maeneo ya nyanda za juu ya Bonde la Ufa kabla ya
mbio za marathon za jijini London mnamo mwezi Aprili, ambazo zitakuwa
zake za kwanza kabisa katika taaluma yake ya riadha.

Mwanariadha huyo mzaliwa wa Somalia, atafanya mazoezi yake katika eneo
la Iten, ambako amejiunga na wanariadha wengine sita wa Uingereza ambao
waliwasili nchini humo mapema mwezi huu kujiandaa kwa Michezo ya Jumuiya
ya Madola itakayoandaliwa mjini Glasgow mwezi Agosti. Wanariadha hao
wanaishi katika kambi ya mazoezi ya nyanda za juu inayomilikiwa na
mzaliwa wa Kenya aliyewahi kuweka rekodi ya ulimwengu ya mbio za half
marathon, Lorna Kiplagat. Mji wa Iten ni nyumbani kwa wanariadha maarufu
wa marathon nchini Kenya ikiwa ni pamoja na Wilson Kipsang, ambaye
ndiye anayeshikilia rekodi ya sasa ulimwenguni kwa upande wa wanaume.
Na wakati Farah na wenzake wakiendelea kuipasha misuli moto, naye gwiji
wa Ethiopia Kenenisa Bekele tayari ana rekodi mbili za ulimwengu, lakini
anasema anaimezea mate rekodi nyingine ya tatu: ambayo mara hii ni ya
mbio za marathon.
Bekele atazitimka mbio za marathon za mjini Paris mnamo Aprili 6, ikiwa
ni wiki moja tu, kabla ya hasimu wake wa uwanjani Mo Farah wa Uingereua
kujitosa barabarani kwa mara ya kwanza katika mbio za marathon. Wote
wawili watalenga kufuata nyayo za Mfalme wa Ethiopia Haile Gebreselassie
na wengine waliofanikiwa kujipa changamoto ya kushiriki mbio za
marathon
0 Komentar untuk "Mwanariadha Mo Farah aendelea na mazoezi Kenya"