Monday, June 9, 2014
Maafisa wa Qatar wanaaminika kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na tishio la kupokonywa uenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa Qatar 2022 kufuatia tuhuma za rushwa .
Kamati andalizi ya michezo hiyo sasa inaaminika kupania kufanya kila iwezalo ikiwemo kufuata mkondo wa kisheria, ikiwa kura ya kuchagua mwandalizi wa kombe la dunia 2022,itarudiwa.
Rais wa Fifa akwepa maswali kuhusu hongo katika uteuzi wa Qatar 2022Shutuma za ufisadi katika mchakato wa kupiga kura ya uwenyeji zilisababisha kuitishwa kwa kura nyingine ikiwa hila itaonekana kuwa ilifanyika.
Qatar inakana shutma za hongo.
Hata hivyo hatma yake imo mikononi mwa mchunguzi wa FIFA,Michael Garcia.
Mwanasheria huyo kutoka Marekani anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake itimiapo Juni 9.
Rais wa Uefa, Michel Platini, aliyeipigia kura Qatari, alisema kuwa atakubali kufanyike kura ya marudio iwapo shutma za ufisadi dhidi ya Qatari zitathibitishwa.
Msimamo wake uko sawa na ule wa makamu wa rais wa Fifa, Jim Boyce aliyesema kuwa hatakuwa na shida yoyote ikiwa ‘makubaliano yatakuwa ni kura ya marudio kufanywa.’
Tag :
soccer
0 Komentar untuk "Angalia Qatar walivyojiandaa kwa viwanja vyenye hadhi kubwa. Qatar kwenda kortini kuhusu kupokonywa uenyeji wa kombe la dunia 2022."