Click here and get some

MTOTO WA ALIEKUA MTABIRI MKUBWA NCHINI ASEMA "WIMBI LA WASANII KUFA LITAENDELEA HADI MWAKANI APRIL NA KUTAJA BAADHI YA MAJINA YA WANAOFUATIA BAADA YA MZEE SMALL"

HASSAN Yahya Hussein ‘Maalim Hassan’ ni mtoto wa pili kati ya wanafamilia, wa kwanza alikuwa wa kike. Mila za kiafrika ndizo zilisababisha arithishwe kazi ya utabiri mara baada ya baba yake mnajimu Shehe Yahya Hussein kufariki dunia.

Maalim Hassan Hussein akiwa ndani ya ofisi za Global Publishers. 
  Maalim alianza kujishughulisha na shughuli za unajimu (astrology) baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha nne na cha sita nchini Kenya.
Awali, ndoto yake haikuwa kufanya kazi za kinajimu, alitaka kuwa wakili au pairoti na ndiyo masomo aliyokuwa akiyapenda.

Akizungumza live mbele ya waandishi wa habari wa Global Publishers mwishoni mwa wiki iliyopita, Maalim alisema alipomaliza kidato cha sita nchini Kenya, marehemu baba yake wakati huo akiwa hai, alimuomba arudi nyumbani Tanzania ili aje kumsaidia kazi za kinajimu.
Alisema baba yake alimfundisha namna ya kufanya kazi hiyo ya kinajimu, baadaye akawa mjuzi kama au zaidi ya alivyokuwa baba yake.
Kwenye mahojiano hayo, Maalim alifunguka mambo mengi yahusuyo unajimu.
Mwandishi: Kuna uhusiano wowote kati ya unajimu na masuala ya uganga?
Maalim: Hakuna uhusiano wowote kati ya unajimu na uganga wa kienyeji.



 
Maalim Hassan Hussein akitoa utabiri ni kwa muda gani vifo vya wasanii vitakavyozidi kudumu.
Astrology ni sayansi ambayo unaweza kuisomea darasani na kuhitimu kabisa katika vyuo vikuu kule Ulaya. Astrology imegawanyika, kuna palmistry (kusoma viganja vya mikono), horoscope (nyota) new roman’s (tafsiri za ndoto) tofauti na waganga ambao wanatumia tunguri na kupiga manyanga. Kazi yangu mimi unaweza kuifananisha na utabiri wa hali ya hewa, watu wa hali ya hewa wanaweza kujua mvua itanyesha lini.
Mwandishi: Kigezo gani mnatumia katika kutabiri?
Maalim: Natumia zaidi mambo ya kimahesabu, namba kila mtu anatumia. Namba zinatuongoza. Kwa mfano mwaka huu ulianza siku ya Jumatano,

tarehe moja inatawaliwa na vitu na sayari fulani, sasa ile sayari kutokana na mambo fulanifulani nikikaa au nikiangalia namba zangu zinavyokaa basi najua mwaka huu kutatokea conflict (mgongano) kati ya hili na hili, sasa hapo ndiyo naweza nikasema kwamba mwaka huu linaweza likatokea jambo fulani.
Mwandishi: Utabiri wako wa vifo vya wasanii umeonekana kutimia, sasa pengine utuambie vifo vitasimama au vitaendelea?
Maalim: Mwaka wa kinyota unaanza mwezi wanne, unaishia mwezi wanne sasa niwathibitishie kwamba hii ‘trend’ ya wasanii kufa itaendelea hadi mwezi wa nne mwaka ujao.
Mwandishi: Watu wanapokufa wewe huwa unajisikiaje na nini kifanyike kuepusha vifo hivyo?
Maalim: Huwa hata mimi sijisikii vizuri lakini kimomoyo huwa nasema ni sawa kwani utabiri wangu umetimia.

Wasanii ambao ndiyo ‘target’ wanatakiwa kuwa na tahadhari, sayari ya Vines inahusiana na masula ya wasanii, sababu inayofanya wasanii wanapoteapotea ni kwa sababu ipo katika conflict na sayari ya Mars. Sayari ya Mars ambayo malaika wake anaiongoza ndiyo Israel ndiye anatoa roho.
Hapa wasanii wanatakiwa kujihami, Mars ni nyekundu, wasanii wajiepushe na vitu vyenye rangi nyekundu kama ‘nail polish’, lipstick na vitu vingine, siyo rangi nzuri kwa wakati huu.
Mwandishi: Huogopi watu wanaweza kukupiga haswa wale wafiwa ambao umetabiri na ndugu zao wakafariki?



Maalim: Mimi siogopi kwa sababu utabiri wangu kama nilivyosema simlengi mtu, nazungumza kwa jamii fulani duniani. Sasa kama watu watakuja kunifanyia fujo sababu ndugu zao wamefariki, basi mimi nitawaangalia lakini sheria zipo, serikali itanilinda.
Mwandishi: Inasemekana wateja wako ni wanawake zaidi, kwa nini?
Maalim: Eeh! Asilimia tisini ya wateja wangu ni wanawake, sijui kwa nini na ndiyo watabiri wengi wanakuwa na wake zaidi ya mmoja…hata huyu mke wangu wa sasa ninayeishinaye nimempata humohumo.

Mwandishi: Watu wanahisi wewe ni Freemason maana umekuwa ukifafanua sana mambo hayo, ni kweli?
Maalim: Watu wanachanganya, watu wanafikiri ni ushirikina. Hamna kitu kama hicho, Freemason ni taasisi zilizoanzishwa na watu fulani kwa ajili ya kusaidia jamii fulani. Wanakutana na kuzungumza masuala yao ya kimaisha na si vinginevyo.

Mwandishi: Kuna uhusiano wowote kati ya majini na unajimu?
Maalim: Majini ni viumbe…katika Kuruani Mwenyezi Mungu anasema tushirikiane nao. Mzee wangu alivyoniambia, kila mtu ukizaliwa lazima utakuwa na jini.

Ratio (uwiano) ya majini ni binadamu mmoja kwa majini 300, wapo watu wanatumia majini kujiingizia fedha. Ni namna ambavyo mtu umepanga kuyatumia lakini si mapepo, mapepo ndiyo mabaya.
 
0 Komentar untuk "MTOTO WA ALIEKUA MTABIRI MKUBWA NCHINI ASEMA "WIMBI LA WASANII KUFA LITAENDELEA HADI MWAKANI APRIL NA KUTAJA BAADHI YA MAJINA YA WANAOFUATIA BAADA YA MZEE SMALL" "

Back To Top