Click here and get some

Arsenal washauriwa watumie pesa nyingi sokoni

Difenda Laurent Koscielny anaamini kocha Arsene Wenger atawezesha Arsenal kutamba tena, ikiwa atanunua angalau wachezaji wanne – ikiwa ni pamoja na straika nyota – majira haya ya joto.
Arsenal, walioshinda Kombe la FA na kufikisha kikomo ukame wa muda mrefu wa mataji, waliongoza Ligi ya Premia vipindi virefu na walikuwa katika nambari mbili za juu kutoka Septemba hadi Machi kabla ya kuteleza na kutua nambari nne baada ya kuaibishwa na wapinzani wao : 5-1 wakiwa Liverpool na 6-0 wakiwa Chelsea.
Vichapo hivi, pamoja na kuumia kwa viungo wa kati Aaron Ramsey na Jack Wilshere, vilifichua udhaifu wa kikosi cha Arsenal.
Kwenye mahojiano na Associated Press katika kambi ya mazoezi ya Ufaransa ya Kombe la Dunia Alhamisi, Koscielny alisema, "Ni muhimu kuwa na angalau wachezaji hawa wanne ili tuweze kukabiliana na timu nyingine.”
Tag : soccer, sports
0 Komentar untuk "Arsenal washauriwa watumie pesa nyingi sokoni"

Back To Top