00:54 Mechi hii imekamilika Brazil ikisajili ushindi mkubwa wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia.
00:52 Oscar amhakikishia kocha Luiz Felipe Scolari ushindi muhimu katika mechi ya ufunguzi wa dhidi ya Croatia
00:51 BAO !! Brazil 3-1 Croatia
00:47 Neymar anaondoka na sasa mchezaji wa Chelsea Ramires anaingia zikiwa zimesalia dakika mbili ya mechi hii.Brazil bado wanaongoza Croatia 2-1
00:45 Brazil wanalazimika kufanya kazi ya ziada kuzima mashambulizi ya Croatia
00:44 Mashambulizi ya Croatia yanazimwa na naibu mkufunzi anayeinua kibendera chake na kuipa Brazil Freekick.
00:43 Bao la Croatia limekataliwa na refarii Yuichi Nishimura
00:40 Maswali yanaibuka kuhusiana na mkwaju huo wa penalti je ulipaswa kupeanwa ama Fred alijiangusha mwenyewe ?
00:37 Zimesalia dakika 13 pekee kabla ya kukamilika kwa mechi hii Brazil 2-1 Croatia .
00:36 David Luiz akosa nafasi nyengine nzuri ya kuongeza bao la tatu dhidi ya Croatia .
00:36 Kona nyengine kwa Brazil.
00:31 Brazil 2-1 Croatia
00:31Neymar afunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.
00:30 Penalti kwa Brazil.Wachezaji wa Croatia wamzunguka Refarii wakilalamikia kuwa haifai kuwa penalti
00:29 Kocha Scolari amuondoa Hulk uwanjani baada ya CRoatia kuanza kuopnesha makeke katika safu ya kati
00:24 Paulinho anaondoka uwanjani . Hermanes anaingia.
00:23 Kocha wa Brazil Scolari naye anafanya badiliko lake la kwanza baada ya dakika 63 ya mechi hii ya kwanza ya Brazil 2014.
00:20 Mabadiliko ya kwanza yanafanywa na Croatia . Mercelo Brozovic anaingia uwanjani badala yake Mateo Kovacic.
00:19 Shabiki sugu wa the Indomitable Lions anasema matokeo ya leo hayamhusu . Kijuu Lubuva ''kwaleo sina timu yangu nikesho cameron 2 mxco 1,nyie mtaona!
00:14 Croatia inaishambulia Brazil lakini hawamakiniki kwenda mbele.
00:10 Neymar anapewa jukumu la kupiga mkwaju mwengine wa Freekick
00:07 Kipindi cha pili kimeanza .Matokeo bado ni Brazil 1-1 Croatia.
11:52 Brazil ndiyo timu ya pekee kuwahi kushiriki fainali zote 20 za Kombe la dunia.
11:52 Mercelo ndiye mchezaji wa kwanza wa Brazil kuwahi kujifunga bao mwenyewe katika kombe la dunia.
11:48 Kipindi cha kwanza kimekamilika mabao yakisalia kuwa ni Brazil 1-1 Croatia
11:45 Mechi ya ufunguzi baina ya Wenyeji Brazil na Croatiabado ni sare ya 1-1 zikiwa zimesalia dakika mbili kipindi cha kwanza kikamilike.
11:44 Mstari huu ni baadhi tu ya mbinu ya kuhakikisha usawa unafanyika katika mechi za kombe la dunia.
11:42 Refarii anatumia rangi nyeupe kuchora mstari kabla ya mkwaju wa freekick kupigwa na Neymar.
11:38 Kocha Luiz Felipe Scolari alalamikia refarii kwa kupeana mpira kwa Croatia ambao alidhania unafaa kuwa wa Brazil
11:36 Kona ya kwanza kwa Croatia .
11:32:
11:30 BAO ! Brazil 1-1 Croatia Neymar
11:29 Neymar ndiye mchezaji wa kwanza kuoneshwa kadi ya Njano kwa kumpiga kumbo Modric
11:20 Paulinho aishambulia lango la Brazil lakini kipa wa Croatia Pletikosa autema.
11:19 Kona ya pili. Neymar anaupiga tena.
11:18 Iwapo mechi hii itaisha Brazil watakuwa wenyeji wa kwanza kuwahi kushindwa katika mechi ya ufunguzi .
11:13 Croatia 1-0 Brazil
11:12 Mercelo ajifunga mwenyewe na kuipa Croatia uongozi wa bao la kwanza .
11:10 Kona ya kwanza katika mechi hii ya ufunguzi inachukuliwa na Neymer.
11:07 Croatia wapoteza nafasi ya wazi kufunga bao la kwanza .
11:00 Mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia imeanza.
10:20 Croatia: Pletikosa; Srna, Ćorluka, Lovren, Vrsaljko; Modrić, Rakitić, Perišić, Brozović; Olić, Jelavić
10:20 Brazil: Cesar; D.Alves, T.Silva, D.Luiz, Marcelo; Paulinho, L.Gustavo; Hulk, Oscar, Neymar; Fred.
10:18Timu zote yaani Brazil na Croatia zimetoa vikozi vyao .
10:15 Timu zote zaingia Uwanjani tayari kwa mechi ya Ufunguzi .
9:40 Usalama umeimarishwa nje ya uwanja wa Sao Paolo
9:35 Mpira ambao ulikuwa kwa wakati huu wote katikati ya uwanja huu unachanuka na sasa ni jukwaa la mwimbaji wa kimataifa Jennipher Lopez kuzindua ukurasa wa muziki.
9:33 Bendera ya Brazil imeingia uwanjani rasmi kama bendera ya taifa mwenyeji wa dimba la mwaka huu wa 2014.
9:31 Vijana wakiwa na mipira na vibendera kutoka mataifa yote yanayoshiriki fainali ya dimba hili wakionesha mbwembwe .
9:30 sherehe ya maadhimisho ya Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 imeanza rasmi katika uwanja wa Sao Paolo.
0 Komentar untuk "Neymar na Oscar waipatia ushindi Brazil ila chamoto wakiona kutoka kwa timu pinzani. Brazil 3-1 Croatia"