Hadi hii leo Divas maarufu waliowahi kufunguka kiundani kuhusu kutoka na
mwanamuziki huyu, na kwa nyakati tofauti kila mmoja wao alijaribu
kufunguka kuhusu experience zao, pindi walipokuwa wanatoka na mkali wa
bongo fleva nchini hivi sasa Mr.Dangote aka Diamond Platnumz, ambaye
amerudiana na kuendelea kudumu katika penzi lake la zamani na la siku
zote kwa Diva Wema Sepetu..basi haya ndo machache waliowahi kutoa ya
moyoni.
DVJ Penny
“Kama uhusiano wowote ulivyo, kuna mwanzo na mwisho na watu wanaachana
kwa sababu nyingi. Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi, wote ni vijana
na wakati mwingine tunahitaji nafasi kugundua vitu vipya, kuona kipi
hasa unachokihitaji kwenye maisha. Unajua ukimruhusu ndege afanye vitu
mbalimbali then atajua kama ‘mti huu ndio
unanifaa, mti huu haunifai. Hivyo nilihisi kwamba wote tulihitaji hicho,
tulihitaji ‘space’ hivyo nikampa nafasi na mimi nakuchukua nafasi. Huwa
nawaambia watu kuwa vyovyote ilivyo, yeyote atakayekuwa naye, nipo
pembeni yake nikimshangilia kwasababu ni kweli (Diamond) ni mtu mzuri
ndani. Achana na watu wanavyomuona chizi chizi, sahau msanii unayemjua,
ana roho nzuri na anajua anachokitaka. Ni ngumu kuacha iende.. kama ni
rahisi kuacha iende basi hujampenda huyo mtu.”
Jokate Mwegelo
“Mahusiano ya diamond yalikuwa very strange, I dont know yani..i think
ilikuwa kazi lakini I guess it was a time I guess I was
frustrated,sielewi yani ilitokea tokea tu”
Jackline Wolper
“Ni kweli niliwahi kuwa na diamond,tulikuwa na mahusiano lakini pia
alikuwa ni mshirika wa biashara,yeye alikuwa hawezi kulala bila
kuniona,lakini tulidumu kama mwezi mmoja hivi, tukaishia kuwa marafiki
tu.
Tag :
Gossip stories
0 Komentar untuk "PENY,JOKATE NA WOLPER WATOA SABABU ZILIZO WAFANYA KUACHWA NA DIAMOND,SOMA HAPA "